Ijumaa, 9 Machi 2018

BREAKING NEWS:MOTO WATETEKEZA BWENI LA WANAFUNZI KIFARU SEC MWANGA


Na Kija Elias, Mwanga.
MOTO mkubwa ambao chanzo chake hakijafahamika hadi sasa umezuka kwenye bweni la  wanafunzi wa Kiume katika shule ya sekondari ya Kifaru iliyopo wilayani Mwanga mkoani kilimanjaro na kuliteketeza kabisa  kusababisha uharibifu mkubwa wa mali.
Mkuu wa wilaya ya Mwanga na mwenyekiti wa  Kamati ya Ulimzi na Usalama ya Wilaya  Aaron Mbogho amedhitisha kutokea kwa tukio hilo    na kwamba hakuna kilichookolewa katika tukio hilo.
Amesa hali hiyo imetokana na Halmashauri ya wilaya ya Mwanga kutokuwa na gari la Zimamoto hatua ambayo ilichangia bweni hilo kuteketea kabisa licha ya juhudi zilizofanywa na wanafunzi na wananchi wanaoishi jirani na hsule hiyo kuzima moto huo bila mafanikio.

Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya mwanga, moto huo ulianza majira ya saa nne na nusu asubuhi jana wakati wanafunzi hao wakiwa madarasani wakiendelea na masomo yao, ghafla moto huo, ulianza kuwaka katika bweni hilo la wanafunzi.

“Ni kweli kuna tukio hilo limetokea majira ya saa nne na nusu asubuhi katika shule ya sekondari Kifaru japokuwa hadi sasa hatujafahamu chanzo chake, tayari nimekwisha kuunda kamati ambayo itachunguza chanzo hicho na kutoa majibu,”alisema

Hilo ni tukio la pili kutokea ndnai ya wiki moja katika wilaya ya Mwanga kwa mabweni ya wanafunzi kuungua moto kwani wiki moja iliyopita  bweni la wanafunzi wa kiume katika shule ya sekondari ya Kwangu liliungua na kuteketea kwa moto japo hapakuwa na madhara kwa wanafunzi.

“Hili ni tukio la pili sasa kutokea ndani ya wiki moja, jumamosi ya tarehe tatu kuna bweni la wavulana katika shule ya sekondari ya Kwangu liliungua moto, leo tena katika shule ya sekondari ya Kifaru bweni limeteketea kwa moto tena,”alisema.

 Bweni la Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kifaru iliyopo wilayani Mwanga likiwa limeteketea kwa moto,mali zote za wanafunzi zimeteketea na hakuna kilichookolewa kwa  mujibu wa Mkuu wa wilaya hiyo,Aaron Mbogho

“Bweni lililoungungua linatumiwa na wanafunzi wa kiume ambalo linauwezo wa kubeba wanafunzi 71, bweni hili linatumiwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne limeteketea kwa moto lote na mpaka sasa hatujajua chanzo chake kama ni umeme au la,”alisema.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kileo Kuria Msuya, ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kila wilaya kuwa na gari la zima moto ambalo litasaidia katika matukio ya moto yanapotokea kuwahi kwenda kuzima.
“Halmashauri nyingi za wilaya hazina vyombo vya zima moto ni vyema serikali kuu kuzisaidia halmashauri ambazo hazina magari ya zima moto,”alisisitiza Msuya.
Diwani huyo amesema kuwa makusanyo ya fedha za ndani za halmashauri haziwezi kutosheleza kununu gari la zima moto hivyo akaiomba tuiombe serikali kuu kuziwezesha halmashauri za wilaya kuwa na gari la zima moto.
“Tumefanya jitihada za kunusuru vitu vya wanafunzi lakini tulishindwa kutokana na kutokuwa na vifaa vya kuzimia moto, kutokana na moto huo kuwa mkali hali ambayo ilipelekea vifaa vyote vya wanafunzi hao kuteketea kwa moto ,”alisema Msuya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni