NA KIJA ELIAS, MOSHI.
Mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA), imewasitishia huduma ya maji safi na salama wakazi zaidi ya 1,503, kutokana na kushindwa kulipa malimbikkizo ya ankara za maji wanayodaiwa na Mamlaka hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habati hivi karibuni,Mkurugenzi wa
Mamalaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi Joyce Msiru alisema
kuwa wateja hao wanadaiwa zaidi ya shilingi Milioni 143.7.
Alikuwa akizungumza kuelekea maadhimisho ya wiki ya maji ambayo
huadhimishwa kila mwaka nchini kote kuanzia machi 16 hadi 22 ambako alitumia muda huo kuwaasa wateja wenye
madeni kulipa ankara zao ili kukwepa adha ya kusitishiwa huduma hiyo mhimu .
Alisema katika kuadhimishi wiki ya maji mjini hapa Mamlaka hiyo
inakusudia kufanya promosheni mbali mbali kwa wateja wake
watakaounganishiwa huduma ya maji safi na maji taka wakiwemo
waliositishiwa huduma ya maji kutokana na malimbikizo ya ankara za maji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na uondoshaji wa maji taka Moshi Mjini(MUWSA),Joyce Msiru akipanda mti ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya maji inayoadhimishwa kila mwaka kuanzia machi 16 hadi 22.
“Tutakuwa na wiki ya maji, wateja wa maji safi ambao watalipa
madeni yao katika wiki ya maji watasamehewa faini ya shilingi 20,000 za
kurudishiwa huduma ya maji majumbani mwao na kwa wale watakaohitaji
kuunganishiwa huduma ya maji taka watalazimika kulipia nusu ya gharama
zinazohitaji na sehemu iliyobaki wataendelea kulipa kwa awamu,”alisema.
Akizungumzia wiki ya maji Mkurugenzi huyo alisema itakwenda pamoja
na zoezi la usafi wa mazingira katika soko la Manyema mjini hapa,kuwa na
maonyesho ya shughuli mbali mbali zinazofanywa na Muwsa ikiwemo utoaji wa elimu
kwa watumiaji wa maji na kuendesha zoezi la upandaji wa miti zaidi ya 12,000
katika vyanzo mbali mbali vya maji mjini hapa.
Meneja biashara wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira John
Ndetico, alisema Mamlaka hiyo inakusudia kuzikatia huduma ya kupata maji
safi taasisi za serikali ikiwemo Ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani
hapa (RPC)Jeshi la magereza na shule ya mafunzo ya awali ya polisi
(CCP) iliyopo mjini hapa.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akipanda mti kuashiria uzinduzi wa wiki ya maji mjini Moshi
Alisema licha ya serikali kuahidi kuzilipitia taasisi hizo madeni
hayo bado zinaendelea kulimbikiza madeni yao na kwamba Muwsa tayari
imeshaziandikia baraua za kuziarifu kuzisitishia huduma ya kupata maji safi.
‘Taasisi hizo zilikuwa zinadaiwa malimbikizo ya zaidi ya shilingi
320 milioni lakini madeni hayo yameongezeka hadi kufikia Julai 2017 bilioni 1.8
na kwamba taasisi hizo hazionyeshi nia ya kulipa malimbikizo hayo licha ya
serikali kuahidi kuzilipia madeni yao yanayoishia june 2017 ambapo kupitia
hazina madai hayo yapo kwenye zoezi la uhakiki ili yaweze kulipwa”alisema
Ndetiko.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba(wa pili kutoka kulia) akikatra utepe kuzindua mfumo wa malipo ya huduma za majisafi na majitaka kupitia NMB Mobile ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya maji.
TUNATEKELEZA: pichani ni Florah Nguma,kaimu ofisa uhusiano MUWSA akipanda mti katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya maji ambayo uliofanyika mjini moshi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni