Jumamosi, 3 Machi 2018

NYUMBA ZILIZOJENGWA NDANI YA HIFADHI MPAKA WA TANZANIA NA KENYA KUVUNJWA,WAPEWA SIKU 20 KUZIBOMOA WENYEWE


Na Kija Elias, Rombo

WIZARA  ya Aridhi,nyumba na maendeleo ya makazi,imetoa muda wa siku 20 kwa wananchi wa mikoa ya Mara,Arusha,Kilimanjaro na Tanga ambao kwa miaka nenda rudi wamevamia na kujenga makazi ya kudumu ndani ya eneo la hifadhi ya mpaka kati ya Tanzania na Kenya.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula baada ya kutembelea eneo la mpaka kati ya Tanzania na Kenya katika tarafa ya Tarakea wilaya ya Rombo inayopapakana na Kenya ambako alishuhudia majumba ya kifahari yakiwa yamejengwa ndani ya eneo la hifadhi ya mpaka.

Mabula alikuwa mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku mbili ambako pamoja na mambo mengine alitembelea eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya ikiwa ni mkakati wa serikali za Tanzania na Kenya kuhakiki mipaka yake kwa kuweka bicorn mpya.
 Naibu Waziri wa Ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi,Angelina Mabula(kushoto)akikagua mawe yaliyopo katika mpaka wa Tanzania na kenya wilayani Rombo,kulia ni Kanoni Masanja ambaye ni katibu Tawala msaidizi Sekretarieti ya mkoa wa kilimanjaro anayeshughulikia miundombinu.

Akizungumza na wavamizi hao,Mabula alisema baada ya muda kumalizika bila wananchi hao kubomoa nyumba hizo,serikali itazibomoa ili kupisha uhakiki wa mpaka huo zoezi ambalo linatekelezwa kwa ushirikiano wa nchi hizo mbili.

Katika ziara hiyo waziri Mabula alitembelea vijiji vya  Mbomai, Nayeme na Leto vyote vikiwa katika tarafa ya Tarakea  wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.

“Serikali imepata fedha kiasi cha shilingi Bilioni 4 kwa ajili ya kurekebisha mipaka yetu ambayo imeonekana kuvunjika, kuharibika na mingine kuwa na umbali mrefu, na haya ni makubaliano yaliyofikiwa kwa nchi mbili Tanzania na kenya,”alisema Naibu waziri Mabula.

Alisema tayari maofisa wa Kenya na Tanzania wanaohisika na utambuzi wa mipata  wamesha kaa  vikao vyao vya awali na kukubaliana kazi hiyo kuanza ramsi machi 22 mwaka huu, ambapo kazi hiyo itaanza kwa kuondoa  bicorn zilizovunjika na kuweka mpya .

“Tunakusudia umbali wa bicorn moja hadi nyingine ziwe karibu kwani za awali zilikuwa mbali sana hali iliyosababisha wananchi hususa wa upande wa Tanzania kulivamia eneo hilo na kujenga makazi yao ya kudumu jambo ambalo halikubaliki.

Hivi karibuni,serikali iliweka alama za X kwa wananchi walioingia na kujenga makazi ya kudumu ndani ya eneo la hifadhi ya mipaka katika mikoa inayopakana na Kenya ambayo ni Mara,Arusha,Kilimanjaro na Tanga mabako Waziri Mkuu kassimu Majliwa aliagiza wavamizi hao kuondeko mara moja.
 Moja ya nyumba za kisasa na bora kabisa iliyojengwa ndnia ya hifadhi ya mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la tarakea wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro,serikali imetoa siku 20 kwa wavanizi hao kubomoa nyumba zao wenyewe kupisha uboreshaji wa mpaka huo.

Kwa mujibu wa waziri Mabula,uwekaji huo wa bicorn mpya utaenda sanjari na zoezi la kusafisha eneo lote la wazi la hifadhi ya mipaka ili kutoruhusu uvamizi utakaofanywa na wananchi.

“Niwaombe wananchi mliovamia eneo hili muondoke mara moja na ifikapo machi 20 mwaka huu kama hamjabomoa nyumba zenu,serikali itazibomoa na agizo la waziri Mkuu la kuwataka  mliovamia eneo la mpaka huo kuondoka linabaki pale pale na mimi nitoa maagizo hapa tena ifikapo Machi 20 wale wote waliojenga katika mpaka huu waanze kuondoka,”alisisitiza .

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Rombo Agnes Hokororo alisema amekubaliana na utekelezaji wa agizo hilo kwa kuwa jambo hilo linaathiri shughuli za mipakani kwa pande zote mbili. 

 Nyumba hii nayo itavunjwa kwani imejengwa ndani ya hifadhi ya mpaka wa Tanzania na Kenya huko Tarakaea wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro,hiki ni kilio kingine kwa wananchi wasiozingatia sheria.
 na hii itavunjwa,nayo imejengwa ndani ya hifadhi ya mpaka huko Tarakea Rombo.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya makazi(katikati),Angelina Mabula akikagua eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro hivi karibuni.
 Naibu waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya kamazi(aliyeshika jiwe)akiwa katika ziara ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya wilayani Rombo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni