NA CHARLES NDAGULLA,MOSHI
MKOA wa Kilimanjaro,umekumbwa
na tishio la ugonjwa wa kichaa cha mbwa ambako mpaka sasa watu watatu wamekufa
kutokana na kung’atwa na mbwa wanaoaminika kuwa na ugonjwa huo wakiwamo watoto
wawili na mama mmoja .
Mbali na watu hao kufariki dunia
katika halmashauri ya wilaya ya Moshi,watu 64 wameripotiwa kujeruhiwa na mbwa
hao wenye ugonjwa wa kichaa cha mbwa katika Vijiji vya TPC,Mawala,Oria,Mabogini
na Ngasini.
Waliofariki dunia kwa kung’atwa na
mbwa hao wametajwa kuwa ni Lulu Zephania(4),Grace Benny (5) mwanafunzi wa shule
ya awali katika shule ya msingi Mawala na Naomi Mmanga(34) wote wakazi wa
Kijiji cha Mawala.
Kwa mujibu wa Dk.Walter
Marandu,daktari wa mifugo katika Halmashauri ya wilaya ya Moshi ,watu hao
walishambuliwa na mbwa mmoja kati ya februari mosi na februari 5 mwaka huu na
kukimbizwa katika Zanahati ya mawala kwa matibabu.
Akizungumza na Ndagullablog,Marandu
amesema kuwa baada ya hali zao kuendelea kuwa mbaya walihamishiwa
katika Hospitali ya TPC inayomilikiwa na Kiwanda cha sukari cha TPC kabla
ya kupelekwa katika Hospital ya rufaa ya KCMC ambako mauti yaliwakuta.
Dk. Marandu amebainisha kuwa,tayari
oparesheni kubwa ya kuwaangamiza mbwa hao inaendelea katika maeneo mbali mbali
yaliyoripotiwa kukumbwa na ugonjwa huo.
Amesema mpaka sasa mbwa zaidi ya 100
wanaodaiwa kuwa na kichaa cha mbwa wameuawa katika oparesheni hiyo katika
vijiji vya Mawala, Mikocheni, Msarikie na Mtakuja.
Kwa mujibu wa Dk.Marandu,watu 64
waliong’atwa na mbwa hao ni katika kipindi cha kuanzia januari hadi mwezi machi
mwaka huu na kwamba tatizo hilo la kuwepo na mbwa wenye kichaa cha mbwa ni
kubwa huku wengi wa mbwa wenye ugonjwa huo ni wale wanaozagaa
mitaani .
Amesema tayari Halmashauri imeanza
kutoa elimu kwa wananchi juu ya kukabiliana na mbwa hao kwa kutoa gari la
matangazo ambalo limekuwa likizunguka katika maeneo mbali mbali ya vijiji kutoa
tahadhari hiyo.
“Timu yetu ya wataalamu ipo vijiji
pamoja na gari la matangazo,tunatoa matangazo makanisani na misikitini juu ya
kuwepo na mbwa wenye kichaa cha mbwa na namna ya wanachi kuchukua
hatua”,amesema.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Kijiji
cha Mawala,David Laizer,amezungumza na Ndagullablog
na kueleza kuwa tayari wamewaua mbwa 19 katika kijiji hicho tangu kuripotiwa
kwa mlipuko wa ugonjwa huo .
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya
ya Moshi,Michael Kilawila amezungumza na Ndagullablog
kuhusiana na kuibuka kwa ugonjwa huo na kueleza kuwa tayari zoezi la kuwapa
chanjo mbwa hao limeanza.
Amesema lengo la chanjo hiyo ni
kuhakikisha mbwa hao hawaendelei kuleta madhara kwa binadamu huku chanjo hiyo
ikienda sanjari na kutolewa kwa elimu kwa wannchi juu ya kujilinda na mbwa hao.
“Tunawaomba wenye mbwa wao
kuhakikisha kuwa mbwa wao wanapatiwa chanjo zinazositahili kuanzia chanjo ya
kichaa cha mbwa, pamoja na magonjwa mengine ili kuepusha watu wasiendelee
kupata madhara zaidi.
Moshi
mjini nako hali tete.
Wakati hali ikiwa hivyo katika
Halmshauri ya wilaya ya Moshi Vijijini,tatizo hilo pia limeripotiwa katika
maeneo kadhaa ya mji wa Moshi ambako watu 13 wamelazwa katika Hospital teule ya
St.Joseph ,Hospital ya Rufaa ya KCMC na kituo cha Afya cha Pasua baada ya
kudaiwa kung’atwa na mbwa hao.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Moshi,Michael Mwandezi amedhibitisha kuwepo na tishio la mbwa
kung’ata watu katika manispaa hiyo alipozungumza na wanahabari ofisini kwake
wiki iliyopita.
Amesema mbali na watu hao kulazwa
kutokana na kushambuliwa na mbwa hao,hadi sasa zaidi ya watu 90 wameripotiwa
kung’atwa na mbwa ndani ya manispaa ya Moshi katika kipindi cha kuanzia januari
hadi machi mwaka huu.
“Ni kweli manispaa yetu imekubwa na ugonjwa wa kichaa
cha mbwa na hivi ninavyozungumza tunao wagonjwa ambao wameng’atwa
na mbwa hao na baadhi yao wamefariki dunia japo kwa sasa sina tawimu
sahihi ya idadi ya waliokufa na pia wako wanaoendelea
kupatiwa matibabu katika hosptali zetu”amesema
Kwa mujibu wa mkurugenzi
huyo,Hospital teule ya Mtakatifu Joseph imepokea wagonjwa wanne wakati Hospital
ya rufaa ya KCMC inayoendeshwa na Shirika la Msamalia Mwema(GSF)imepokea
wagonjwa saba na kituo cha Afya cha pasua kinao wagonjwa wawili.
Amesema jitihada mbali mbali
zimechukuliwa kukabilina na tishio la mbwa hao ikiwamo kuendesha oparesheni ya
kuwaua mbwa wote wanaoonekana wakilanda landa mitaani.
”Tumeshaanza kutoa
matangazo kwa wananchi na tumewataka kutoa taarifa endapo watawaona mbwa
wakilanda landa mitaani na pia tumetoa maelekezo kwa wamiliki wa mbwa kuchukua
tahadhari ikiwamo kuwapa chanjo mbwa ”amesema
Mganga Mkuu wa Manispaa
hiyo, Soka Mwakapalala amesema baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika
Hospitali za KCMC na Mtakatifu Joseph hali zao ni mbaya kutokana na
baadhi yao kuripotiwa kupatwa na tatioz la kubweka kama mbwa.
Dk. Mwakapalala amesema kuwa mpaka
sasa watu 91 wameripotiwak ung’atwa nam bwa kati ya januari na machi mwaka huu
huku akieleza kuwa virusi vya kichaa cha mbwa hushambulia sana mishipa ya
fahamu na dalili kubwa ni mtu Kubweka kama mbwa na mwisho mtu
huyo hupoteza fahamu na kufariki.
“Asilimia 99 ya wagonjwa
walioang’atwa na mbwa hufariki dunia hivyo kunahitajika tahadhari kubwa sana na
tunawaomba wananchi pindi wanaposhambuliwa na mbwa ni mhimu kwenda haraka
kupata matibabu ndani ya saa 24”amesema.
Mpaka sasa Manispaa ya Moshi
imeendesha oparesheni na kuwaua mbwa 700 kwa kuwapiga risasi huku mbwa 709
wkaipatiwa chanjo.
Kwa mujibu wa Dk. Mwakapalala,
katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2016 watu zaidi ya 1,000
waling’atwa na mbwa ambapo mwaka 2016 walikuwa 434, mwaka 2017 watu 564
na katika kipindi cha kuanzia January hadi Machi mwaka huu ni watu 91.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni