Na
Kija Elias, Mwanga.
MOTO
mkubwa ambao chanzo chake hakijafahamika hadi sasa umezuka kwenye bweni la wanafunzi wa Kiume katika shule ya sekondari
ya Kifaru iliyopo wilayani Mwanga mkoani kilimanjaro na kuliteketeza kabisa kusababisha uharibifu mkubwa wa mali.
Mkuu
wa wilaya ya Mwanga na mwenyekiti wa Kamati ya Ulimzi na Usalama ya Wilaya Aaron Mbogho amedhitisha kutokea kwa tukio
hilo na kwamba hakuna
kilichookolewa katika tukio hilo.
Amesa
hali hiyo imetokana na Halmashauri ya wilaya ya Mwanga kutokuwa na gari la
Zimamoto hatua ambayo ilichangia bweni hilo kuteketea kabisa licha ya juhudi
zilizofanywa na wanafunzi na wananchi wanaoishi jirani na hsule hiyo kuzima
moto huo bila mafanikio.
Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya mwanga,
moto huo ulianza majira ya saa nne na nusu asubuhi jana wakati wanafunzi hao
wakiwa madarasani wakiendelea na masomo yao, ghafla moto huo, ulianza kuwaka
katika bweni hilo la wanafunzi.
“Ni kweli kuna tukio hilo limetokea majira
ya saa nne na nusu asubuhi katika shule ya sekondari Kifaru japokuwa hadi sasa
hatujafahamu chanzo chake, tayari nimekwisha kuunda kamati ambayo itachunguza
chanzo hicho na kutoa majibu,”alisema
Hilo ni tukio la pili kutokea ndnai ya
wiki moja katika wilaya ya Mwanga kwa mabweni ya wanafunzi kuungua moto kwani
wiki moja iliyopita bweni la wanafunzi
wa kiume katika shule ya sekondari ya Kwangu liliungua na kuteketea kwa moto
japo hapakuwa na madhara kwa wanafunzi.
“Hili ni tukio la pili sasa kutokea ndani
ya wiki moja, jumamosi ya tarehe tatu kuna bweni la wavulana katika shule ya
sekondari ya Kwangu liliungua moto, leo tena katika shule ya sekondari ya
Kifaru bweni limeteketea kwa moto tena,”alisema.
Bweni la Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kifaru iliyopo wilayani Mwanga likiwa limeteketea kwa moto,mali zote za wanafunzi zimeteketea na hakuna kilichookolewa kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya hiyo,Aaron Mbogho
“Bweni lililoungungua linatumiwa na
wanafunzi wa kiume ambalo linauwezo wa kubeba wanafunzi 71, bweni hili linatumiwa
na wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne limeteketea kwa moto lote na
mpaka sasa hatujajua chanzo chake kama ni umeme au la,”alisema.
Kwa
upande wake Diwani wa Kata ya Kileo Kuria Msuya, ameiomba serikali kuangalia
uwezekano wa kila wilaya kuwa na gari la zima moto ambalo litasaidia katika
matukio ya moto yanapotokea kuwahi kwenda kuzima.
“Halmashauri
nyingi za wilaya hazina vyombo vya zima moto ni vyema serikali kuu kuzisaidia
halmashauri ambazo hazina magari ya zima moto,”alisisitiza Msuya.
Diwani
huyo amesema kuwa makusanyo ya fedha za ndani za halmashauri haziwezi kutosheleza
kununu gari la zima moto hivyo akaiomba tuiombe serikali kuu kuziwezesha halmashauri
za wilaya kuwa na gari la zima moto.
“Tumefanya
jitihada za kunusuru vitu vya wanafunzi lakini tulishindwa kutokana na kutokuwa
na vifaa vya kuzimia moto, kutokana na moto huo kuwa mkali hali ambayo
ilipelekea vifaa vyote vya wanafunzi hao kuteketea kwa moto ,”alisema Msuya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni