Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na uondoshaji wa majitaka Moshi Mjini(MUWSA),Joyce Msiru akitoa taarifa ya utendaji kazi wa mamlaka hiyo katika uzinduzi wa wiki ya maji hvi karibini mjini moshi.
MKUU wa Wilaya ya
Moshi Mkoani Kilimanjaro, Kippi Warioba amewataka Wananchi kulipa ankra za maji
kwa wakati, ili huduma hiyo izidi kuwa endelevu, hali ambayo itawezesha pia
kuwahudumia watu wengine kwa pamoja.
Warioba alitoa
kauli hiyo hivi karibuni kwenye uzinduzi
wa Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo kimkoa yalifanyika mjini moshi
katika viwanja vya Mamlaka ya Majisafi
na Uondoshai wa maji taka moshi mjini (MUWSA).
Alisema kuwa ili MUWSA
iweze kuendelea kutoa huduma bora ya maji kwa wananchi wa moshi ni vyema
Wananchi wakawa na utayari wa kulipia ankra hizo kwa wakati.
“Niwaase Wananchi
wenzangu kulipia ankra zenu za maji kwa wakati ili kuifanya huduma ya maji
itolewayo na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira MUWSA, kuwa
endelevu,”alisema Warioba.
Aidha mkuu huyo wa
wilaya aliwataka Wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji, ili maji hayo
yaendelea kuwapo wakati wote kwenye vyanzo vya maji vilivyopo bila kupungua.
“Nachukua nafasi hii
kuwaasa wale wote wanaofanya shughuli za uharibifu wa mazingira kwenye vyanzo
vya maji kuacha mara moja kufanya uharibifu huo,”alisema.
MKuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba(wa pili kutoka kulia)akikata utepe kuzindua huduma mpya ya kulipia ankara za maji ijulikanayo kama NMB Mobile katika uzinduzi wa wiki ya maji iliyofanyika hivi karibuni mjini Moshi.
Aliongeza kuwa “Naomba
nitoe agizo kali kwa yeyote atakayepatikana anafanya shughuli za uharibifu wa
mazingira kwenye vyanzo vya maji, hatua kali zichukuliwe dhidi yake, na wale
wote watakaokwenda kinyume na katazo la sheria hizi, waweze kushughulikiwa kwa
mujibu wa sheria,”alisema.
Kwa mujibu wa mkuu
huyo wa wilaya sheria ya rasilimali za maji namba 11 ya mwaka 2009 kifungu cha
34, sambamba na sheria ya mazingira namba 20 ya mwaka 2004 kifungu cha 57,
vyote kwa pamoja vinapinga kufanyika kwa
shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60
kwenye vyanzo vya maji, mabwawa, mito, maziwa, chemichemi pamoja na kwenye
visima.
Nae Mkurugenzi
mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na ondoshaji wa majitaka(MUWSA) Joyce Msiru,
alisema kuwa Mamlaka hiyo inaendelea kuhamasisha na kuwaelimisha Wananchi
kushiriki kikamilifu katika matumizi ya majisafi na usafi wa
mazingira, ikiambatana na kulipia ankra za matumizi ya majisafi na maji taka
kwa wakati.
“Mamlaka inaendelea
kushirikiana na wadau mbalimbali katika sekta ya maji kuelimisha jamii juu ya
uhifadhi wa vyanzo vya maji na uendeshaji endelevu wa miradi ya maji, ili
kuhakikisha kizazi kijacho kinapata rasilimali ya majisafi kwa uhakika na ubora
unaotakiwa,”alisema Msiru.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni