Anitha Mkazi
wa Karanga Manispaa ya Moshi,alikamatwa desemba 19 mwaka jana akiwa na shehena
ya madawa ya kulevya aina ya mirungi aliyokuwa akiisafrisha kwa kutumia gari
lake dogo aina ya Toyota Sienta lenye namba za usajili T674DLB.
Alikamatwa
na askari wa Doria eneo la Majengo kwa Mtei mjini Moshi akiwa anasafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi
kilo 216 na gramu 370”.
Kutokana
na kuharibika kwa karandinga la polisi,kesi hiyo sasa imepigwa kalenda hadi
machi 27 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa katika mahakama ya hakimu
mkazi mjini Moshi kutokana na upelelezi wa shauri lake kutokamilika.
Katika
kesi hiyo,dereva taksi mkazi wa mjini moshi,Frank Sifael Moshi maarufu kwa jina
la ‘Gaucho’ameunganishwa na Anitha na inadaiwa ndiye aliyekuwa akiendesha gari
la Anitha wakati wa tukio hilo.
Hata hivyo
dereva huyo alitimua mbio baada ya gari hilo kusimamishwa na polisi wa doria na
kumwacha Anitha akiangukia mikononi mwa polisi jaoo naye arobaini yake ilitimia
baada ya kunaswa na polisi.
Anitha Osward,mtuhumiwa wa dawa za kulevya,akiwa mikononi mwa polisi muda mfupi baada ya kukamatwa akituhumiwa kusafrisha shehena ya dawa za kulevya aina ya Morungi.
Hii ndiyo shehena ya dawa za kulevya aina ya mirungi ambayo ilikamatwa ndani ya Gari la Anitha Osward lenye namba za usajili T674DLB aina ya Toyota Sienta,tayari Anitha na dereva wake Frank Sifael Moshi a.k.a Gaucho,wameshafikishwa makahamani wakishitakiwa kwa kosa la kusafrisha dawa za kulevya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni