ASKARI wa shirika la Hifadhi za taifa
nchini(Tanapa)wakishirikiana na askari wa jeshi la polisi nchini,wamefanikiwa
kuwanasa watu wanne wanaotuhumiwa kuwa ni
majangili wanaodaiwa kujihusisha na mauaji ya wanyama katika hifadhi ya Taifa ya
Serengeti(SENAPA).
Taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari kupitia Meneja mawasiliano,Tanapa Pascal Shelutete leo machi
mosi,imeeleza kuwa,miongoni mwa majangili walionaswa ni wale wanaodaiwa kuua
faru katika hifadhi hiyo mwezi Desemba mwaka jana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni