Na Kija Elias, Rombo
WIZARA ya Aridhi,nyumba na
maendeleo ya makazi,imetoa muda wa siku 20 kwa wananchi wa mikoa ya
Mara,Arusha,Kilimanjaro na Tanga ambao kwa miaka nenda rudi wamevamia na
kujenga makazi ya kudumu ndani ya eneo la hifadhi ya mpaka kati ya Tanzania na
Kenya.
Agizo hilo limetolewa na Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula baada ya
kutembelea eneo la mpaka kati ya Tanzania na Kenya katika tarafa ya Tarakea
wilaya ya Rombo inayopapakana na Kenya ambako alishuhudia majumba ya kifahari yakiwa yamejengwa
ndani ya eneo la hifadhi ya mpaka.
Mabula alikuwa mkoani Kilimanjaro
kwa ziara ya siku mbili ambako pamoja na mambo mengine alitembelea eneo la
mpaka wa Tanzania na Kenya ikiwa ni mkakati wa serikali za Tanzania na Kenya
kuhakiki mipaka yake kwa kuweka bicorn mpya.
Naibu Waziri wa Ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi,Angelina Mabula(kushoto)akikagua mawe yaliyopo katika mpaka wa Tanzania na kenya wilayani Rombo,kulia ni Kanoni Masanja ambaye ni katibu Tawala msaidizi Sekretarieti ya mkoa wa kilimanjaro anayeshughulikia miundombinu.
Akizungumza na wavamizi hao,Mabula
alisema baada ya muda kumalizika bila wananchi hao kubomoa nyumba hizo,serikali
itazibomoa ili kupisha uhakiki wa mpaka huo zoezi ambalo linatekelezwa kwa
ushirikiano wa nchi hizo mbili.
Katika ziara hiyo waziri Mabula
alitembelea vijiji vya Mbomai, Nayeme na Leto vyote vikiwa katika tarafa
ya Tarakea wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.
“Serikali imepata fedha kiasi cha
shilingi Bilioni 4 kwa ajili ya kurekebisha mipaka yetu ambayo imeonekana
kuvunjika, kuharibika na mingine kuwa na umbali mrefu, na haya ni makubaliano
yaliyofikiwa kwa nchi mbili Tanzania na kenya,”alisema Naibu waziri Mabula.
Alisema tayari maofisa wa Kenya na
Tanzania wanaohisika na utambuzi wa mipata wamesha kaa vikao vyao
vya awali na kukubaliana kazi hiyo kuanza ramsi machi 22 mwaka huu, ambapo kazi
hiyo itaanza kwa kuondoa bicorn zilizovunjika na kuweka mpya .
“Tunakusudia umbali wa bicorn moja
hadi nyingine ziwe karibu kwani za awali zilikuwa mbali sana hali
iliyosababisha wananchi hususa wa upande wa Tanzania kulivamia eneo hilo na
kujenga makazi yao ya kudumu jambo ambalo halikubaliki.
Hivi karibuni,serikali iliweka alama
za X kwa wananchi walioingia na kujenga makazi ya kudumu ndani ya eneo la
hifadhi ya mipaka katika mikoa inayopakana na Kenya ambayo ni
Mara,Arusha,Kilimanjaro na Tanga mabako Waziri Mkuu kassimu Majliwa aliagiza
wavamizi hao kuondeko mara moja.
Moja ya nyumba za kisasa na bora kabisa iliyojengwa ndnia ya hifadhi ya mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la tarakea wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro,serikali imetoa siku 20 kwa wavanizi hao kubomoa nyumba zao wenyewe kupisha uboreshaji wa mpaka huo.
Kwa mujibu wa waziri Mabula,uwekaji
huo wa bicorn mpya utaenda sanjari na zoezi la kusafisha eneo lote la wazi la
hifadhi ya mipaka ili kutoruhusu uvamizi utakaofanywa na wananchi.
“Niwaombe wananchi mliovamia eneo
hili muondoke mara moja na ifikapo machi 20 mwaka huu kama hamjabomoa nyumba
zenu,serikali itazibomoa na agizo la waziri Mkuu la kuwataka mliovamia
eneo la mpaka huo kuondoka linabaki pale pale na mimi nitoa maagizo hapa tena
ifikapo Machi 20 wale wote waliojenga katika mpaka huu waanze
kuondoka,”alisisitiza .
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya
Rombo Agnes Hokororo alisema amekubaliana na utekelezaji wa agizo hilo kwa kuwa
jambo hilo linaathiri shughuli za mipakani kwa pande zote mbili.
Nyumba hii nayo itavunjwa kwani imejengwa ndani ya hifadhi ya mpaka wa Tanzania na Kenya huko Tarakaea wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro,hiki ni kilio kingine kwa wananchi wasiozingatia sheria.
na hii itavunjwa,nayo imejengwa ndani ya hifadhi ya mpaka huko Tarakea Rombo.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya makazi(katikati),Angelina Mabula akikagua eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro hivi karibuni.
Naibu waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya kamazi(aliyeshika jiwe)akiwa katika ziara ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya wilayani Rombo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni