Alhamisi, 14 Desemba 2017

MIILI YA WANAJESHI WA JWTZ WALIOUAWA NCHINI DRC YAAGWA JIJINI DAR ES SALAAM

Magari ya jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ) yakiwa na miili ya wanajeshi wa jeshi hilo waliouawa nchini DRC hivi karibuni  kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi hilo 'Ngome'Upanga Jijini Dar es salaam ambako miili hiyo iliagwa kwa heshima zote za kijeshi
 Maofisa wa jeshi la wananchi Tanzania(JWTZ)wakiwa wamebeba majeneza yenye  miili ya wanajeshi wa jeshi hilo waliouawa nchini DRC hivi karibuni na waasi wa ADF baada ya kambi ya wanajeshi hao kuvamiwa na waasi hao.
Majeneza yenye miili ya wanajeshi wa JWTZ yakiwa yamepambwa na bendera ya Taifa na ile ya Umoja wa Mataifa(UN) kabla ya shughuli ya kuiaga katika viwanja vya Makao Makuu ya jeshi hilo Upanga Jijijini Dar es salaam.
 Maofisa wa JWTZ wakitoa heshima za mwisho kwa miili ya maofisa wenzao waliouawa nchini DRC hivi karibuni,shughuli za kuaga miili hiyo ilifanyika Jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Makao Makuu ya jeshi hilo 'ngome'Upanga.


 TUTAWAKUMBUKA DAIMA


Sherehe ya kuwaaga wanajeshi 14 wa Tanzania waliokuwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa waliouawa nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo zimefanyika jiji Dar es Salaam.

Wanajeshi hao waliuawa baada ya kupigana na waasi kwa muda wa saa 13 kufuatia waasi hao kuishambulia kambi yao.

Sherehe hizo zimefanyika kwenye makao makuu ya jeshi la ulinzi na usalama Tanzania "gnome" upanga jijini Dar es Salaam

Mkuu wa ulinzi wa amani wa Umoja wa mataifa Jean Piare Lacroix, alihudhuria sherehe hizo. Familia za wanajeshi hao nazo zilikuwepo na zimeungana na wapendwa wao kuelekea mikoani.

Shambulio hilo lilitekelezwa Alhamisi iliyopita kwenye kambi ya jeshi ya Semuliki eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa ilisema wanajeshi 5 wa jeshi la DR Congo (FARDC) waliuawa pia kwenye shambulio hilo.

Umoja wa Mataifa unasema waasi wa ADF ndio wanaotuhumiwa kutekeleza shambulio hilo.





 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni