Jumamosi, 11 Novemba 2017

PRINMAT WALIA KUNYIMWA CHANJO YA KUZUIA MAABUKIZI YA VVU KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO








CHAMA  cha Wauguzi na wakunga walio katika huduma binafsi Tanzania(PRINMAT)kimelalamikia urasimu unaofanywa na serikali wa kuwanyima chanjo ya kuzuia maambukizi ya Virus vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Malalamiko hayo yalitolewa hivi karibuni  mjini moshi na mwenyekiti wa Chama hicho,Keziah Kapesa katika hotuba yake ya ufunguzi kwenye mkutano mkuu wa 17 wa chama hicho unaoendelea mjini hapa.

Alisema zipo baadhi ya wilaya zimeshindwa kutoa friji za chanjo pamoja na vitendanishi kwa vituo vya PRIMAT licha ya kwamba taarifa zote za huduma hupelekwa ofisi za wagaga wakuu wa wilaya.

“Lakini kuna tatizo vituo kadhaa vya wauguzi kukosa fridge za chanjo,wakati wakipata chanjo kutoka vituo vya jirani takwimu zinakwenda huko halmashauri”,alisema.

Katika hotuba yake,mwenyekiti huyo amesema mbali na vituo hivyo kukosa friji za chanjo,pia wauguzi hao na wakunga wamekuwa hawapati mafunzo kazini kwa lengo la kuboresha huduma wanazotoa.

Amesema pamoja na kutopatiwa mafunzo,wakaguzi wamekuwa wakifika kwenye vituo hivyo kwa ajli ya ukaguzi  na kuhoji kwa nini vituo vya prinmat havitoi huduma kwa njia iliyoboreshwa.

Chama hicho pia kimelalamikia hatua ya serikali kuvifungia vituo vya pirnmat bila kutoa sababu za msingi  huku baadhi ya vituo vinavyofungwa vikiwa mbali na hospital za serikali jambo ambalo kimedai linaweza kusababisha madhara makubwa kwa wagonjwa.

Kaimu mkurugenzi wa tiba kutoka wizara ya Afya,Dk.Dorothy Gwajima alisema kuvifugia vituo  vya afya vilivyopo chini ya prinmat  ni kuwanyima huduma wananchi  wasiokuwa na hatia.

Alisema prinmat ni wadua wakubwa wa wizara ya Afya kwani wamesajiliwa na serikali na wanafuata miongozo yote ya serikali hivyo kuvifungia vituo vyao ni jambo lisilokubalika.

Gwajima aliyekuwa mgeni rasmi katika mkutano huo,alisema kuna matatizo yanayoweza kupatiwa ufumbuzi kwa njia ya mazungumzo lakini baadhi ya watumishi wa wizara ya afya wamekuwa wakikuza matatizo kwa makusudi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni