Watu 36 wamepoteza maisha na wengine kiasi ya 40
kujeruhiwa kutokana na mkanyagano katika hekaheka za kusherehekea mwaka mpya
nchini China.
Tukio hilo lilitokea wakati
umati mkubwa wa watu ukiwa umekusanyika katika uwanja wa Chen Yi Square.
Shirika la habari la China Xihnua limemnukuu aliyeshuhudia mkasa huo akisema
watu walikuwa wakitaka kujipatia kuponi ambazo zilionekana kama fedha aina ya
dola ambazo zilikuwa zikirushwa kutoka katika dirisha kutoka gorofa ya tatu ya
jengo moja.
Serikali
ya China iliosema umma huo wa watu ulianza kukanyagana mapema kabla ya kutimia
usiku wa manane, katika mji huo wenye mchanganyiko wa watu. Tukio hilo
linaelezwa kuwa baya zaidi kutokea tangu mwaka 2010, baada ya kuzuka moto
katika jengo lenye makazi ya watu na kusababisha vifo vya watu 58.
Chanzo
cha mkanyagano huo bado hakijafahamika lakini chombo cha habari cha serikali na
baadhi ya walioshuhudia wanasema kwa sehemu fulani kadhia hiyo imesababishwa na
watu wakiwania kujipatia fedha zilizoonekana kama ni sarafu halisi.
CHANZO: DW
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni