Jumatano, 7 Januari 2015

OBAMA AKUTANA NA NIETO WA MEXICO



Rais wa Marekani Barack Obama ameahidi kuisadia Mexico dhidi ya wimbi la machafuko na magenge ya walanguzi wa dawa za kulevya. 

Obama alikutana na rais wa Mexico Enrique Pena Nieto katika ikulu yake mjini Washington jana huku kukiwa na wasiwasi kuhusiana na kutekwa kwa wanafunzi 43 wa Mexico mwezi Septemba mwaka uliopita. 

Waandamanaji kadhaa walikusanyika nje ya ikulu wakitaka kujua kilichotokea kwa wanafunzi hao ambao inachukuliwa walikufa wakiwa mikononi mwa viongozi na maafisa wa polisi wanaoshirikiana na genge la walanguzi wa dawa za kulevya. 

Obama alikabiliwa na shinikizo kutoka kwa makundi ya haki za binadamu likiwemo Human Rights Watch kumshinikiza Pena Nieto atilie maanani zaidi suala hilo la wanafunzi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni