Alhamisi, 29 Januari 2015

MBEYA CITY YAIADIBISHA SIMBA SC, YAIBANJUA 2-1 UWANJA WA TAIFA



 HAJIBU AKIBANWA MBAVU NA WALINZI WA MBEYA CITY FC.


Timu ya soka ya Simba jana ilikwaa kisiki katika michuano ya ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mbeya City.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 23 lililofungwa na mshambuliaji chipukizi Ibrahim Ajibu. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko.

Mbeya City ilisawazisha bao hilo dakika ya 76 kupitiakwa Paul Nonga baada ya kufanyika kwa shambulizi kali kwenye lango la Simba.

Bao la pili na la ushindi la Mbeya City lilifungwa kwa njia ya penalti na Yussuf Abdalla baada ya kipa Manyika Peter wa Simba kudaka mguu wa Raphael Alfa ndani ya mita 18 badala ya mpira.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni