Jumatano, 21 Januari 2015

CHELSEA YAAMBULIA SARE ANFIELD, CAPITAL ONE CUP



Rahim Sterling aliiokoa Liverpool, alipotupia bao lililowapa sare ya 1-1 dhidi ya Chelsea katika Capital One Cup huku wakisubiri mzunguko wa pili watakaotua Stamford Bridge kwa ajili ya kuamua wa kwenda hatua ya mwisho ya michuano hiyo.

Eden Hazard alifumania nyavu kwa mkwaju wa penati bao lililodumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika baada ya Markovic kumuangusha nyota huyo wa Ubelgiji katika eneo la hatari.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni