Timu za soka za Simba na Mtibwa
Sugar, zinatarajiwa kushuka dimbani kesho kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar,
kumenyana katika mechi ya fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Pambano hilo linalosubiriwa kwa
hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini, linatarajiwa kuwa na ushindani mkali
kwa vile kila timu itapania kushinda ili kuibuka na ubingwa.
Simba ilifuzu kucheza fainali
baada ya kuichapa Polisi Zanzibar bao 1-0 wakati Mtibwa Sugar iliitoa JKU kwa
njia ya penalti tano tano baada ya kumaliza dakika 90 zikiwa sare.
Akizungumzia pambano hilo, Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic, alisema hana wasiwasi wa timu yake kutwaa ubingwa.
Akizungumzia pambano hilo, Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic, alisema hana wasiwasi wa timu yake kutwaa ubingwa.
Kocha huyo kutoka Serbia
alisema, timu yake ipo imara na hawana hofu na wapinzani wao kwa vile wana uhakika
mkubwa wa kutwaa ubingwa.
Goran alisema vijana wake wote
wapo katika hali nzuri na wana ari kubwa ya kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa wa
michuano hiyo ya kihistoria.
Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa
Mtibwa Sugar, Mecky Maxime,alisema dakika 90 za mchezo ndizo zitakazoamua
bingwa wa michuano hiyo.
Mecky alisema kikosi chake kipo
mara na kinatambua nini la kufanya katika mechi hiyo na kusisitiza kuwa, hana
hofu na wapinzani wao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni