Ijumaa, 9 Januari 2015

ALBINO WA KWIMBA AIGUSA UN



 ALVARO RODRIGUEZ


Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez amesema Umoja wa Mataifa (UN) umesikitishwa na kitendo cha kuporwa kwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Pendo Emmanuel (4) na watu wasiojulikana kilichotokea katika kijiji cha Ndami wilayani Kwimba mkoani hapa ambapo hadi sasa bado hajapatikana.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jijini Mwanza baada ya kutembelea mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mara, Shinyanga na Mwanza kuangalia miradi inayotekelezwa na Umoja wa Mataifa pamoja na masuala ya haki za binadamu, Alvaro Rodriguez alisema serikali kupitia Mkuu wa mkoa, Magesa Malongo na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Valentino Mokiwa wahakikishe wanaendelea kumtafuta na kulipa suala hilo kipaumbele.

Hadi kufikia jana zilikuwa zimefika siku 13 tangu mtoto huyo aporwe na watu wasiojulikana Desemba 27, mwaka jana katika kijiji cha Ndami, tarafa ya Mwamashinda wilayani Kwimba.

Kwa upande wake, Kamanda Mlowola alisema licha ya jitihada zinazofanywa na Jeshi la Polisi za kumtafuta mtoto Pendo, lakini bado hajapatikana. wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo mwanzo mwa wiki hii alitoa siku tano kwa uongozi wa kijiji cha Ndami, wilayani Kwimba na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanampata mtoto huyo hadi ifikapo leo.

Tayari watu 15 wanashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi wa kuhusika na uporwaji wa mtoto huyo akiwemo baba mzazi, Emmanuel Shilinde.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni