Wazee wasiojiweza
wanaoishi kwenye kambi ya wazee ya Njoro katika Manispaa ya Moshi inayomilikiwa
na serikali kuu wanakabiliwa na matatizo mbali mbali ikiwa ni pamoja na
ukosefu wa huduma za afya,usafiri na uzio wa makazi yao.
Bi. NDETA TENGA
Wazee hao wametoa
malalamiko hayo kwa kikundi cha familia ya wakazi wa Manispaa ya Moshi cha
‘Big Family’ ambao waliitembelea kambi hiyo kuwapa misaada ya kijamii wazee hao
na kula nao chakula cha mchana.
Wakizungumza kwa
niaba ya wenzao Mzee Salim Ali na Mzee Inyasi Atanasi ambaye ni mwenyekiti wa
wazee hao wamesema, ingawa kuna zahanati katika kambi hiyo lakini haina dawa za
kutosha na hamna vipimo wanapougua..
Malalamiko
ya wazee hao yameungwa mkono na Afisa Ustawi Mfawidhi wa kambi hiyo yenye
uwezo wa kuhudumia wazee 35 Bi. Ndeta Tenga na kueleza kuwa wazee wanne
wamefariki dunia kati ya mwezi Januari na Mei mwaka jana na kuiomba
serikali iboreshe huduma za kambi hiyo.
Akiongea
na wazee hao baada ya kukabidhi msaada huo ukiwemo unga, nguo,mafuta ya
kupikia, mchele, sukari, sabuni na viatu vyenye thamani ya zaidi ya shs.
2.5mil/= Mwenyekiti wa ‘Big Family’ Dismas Dede ameahidi kuboresha baadhi ya
huduma ikiwa ni pamoja na kukarabati jiko.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni