Jumanne, 20 Januari 2015

UNAIKUMBUKA MECHI YA CHELSEA WALIPOZABUA LIVERPOOL 3-2 KOMBE LA LIGI 2004/05?



 DIDIER DROGBA AKIWADHIBITI WALINZI WA LIVERPOOL 2009

Jose Mourinho alikuwa akiingia katika soka la England, na kukutana na hali ambayo aliitumia fursa muhimu kwa ajili ya kujipatia ujiko; hii ilikuwa ni michuano ya ligi ikiwa chini ya mdhamini Carling.

Wengi waliitazama michuano ya Carling Cup kama ‘Kombe la Mbuzi’ isiyo na maana yoyote ile kwao, alimpapatua Sir Alex Ferguson kisha Rafa Benitez akiwa Liverpool aliidungua mabao 3-2.

Katika dakika ya kwanza, utamkumbuka John Arne Riise wa Liverpool alitupia bao; lakini hali ilibadilika ghafla Steven Gerrard alipojifunga bao na kuipa ahueni ‘the blues’ hadi muda wa nyongeza ambako Chelsea iliwatungua Liverpool mabao matatu.

Nyota wa Liverpool Anntonio Nunez alitupia bao katika dakika ya 113, lakini bao lake lilikuja mwishoni wakati  Didier Drogba na Mateja Kezman walipotupia mabao.

CHANZO: JAIZMELALEO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni