Polisi wa kupambana na
ugaidi wa Ufaransa wameanzisha operesheni ya kuwasaka washambuliaji waliowaua
watu 12 katika ofisi za jarida la kila wiki la Chalie Hebdo mjini Paris jana.
Waziri mkuu wa Ufaransa
Manuel Valls amesema watu kadhaa wamekamatwa.
Televisheni za Ufaransa
zimewaonyesha walenga shabaha wa kikosi maalumu cha polisi wakiwa katika
barabara za mji wa Reims, huku duru zilizo karibu na operesheni hiyo zikisema
wanaume watatu, wawili kati yao wakiwa ndugu, wametambuliwa kama washukiwa.
Polisi wametoa picha za ndugu hao.
Mmoja wa washukiwa hao
watatu alifungwa jela mwaka 2008 kwa kuhusika na mtandao unaowapeleka
wapiganaji nchini Iraq. Washukiwa wanasemakana kuwa na umri wa miaka 18, 32 na
34.
Taarifa za hivi karibuni
zimeeleza kuwa mmoja wa washukiwa hao amejisalimisha kwa polisi. Zaidi ya watu
100,000 walijitokeza kote Ufaransa kuyapinga mauaji hayo.
Rais wa Ufaransa
Francoise Hollande amelieleza shambulizi hilo kuwa la kigaidi na kutangaza leo
kuwa siku ya maombolezo ya kitaifa.
CHANZO: el Santiago DEL ESTERO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni