Majeshi ya usalama nchini
Ufaransa, jana Ijumaa yakitumia mabomu na bunduki yalifikisha mwisho siku tatu
za ugaidi mjini Paris, wakiwauwa ndugu wawili wenye mahusiano na kundi la
al-Qaeda.
Ndugu
hao walifanya mauaji ya watu 12 katika jarida la vikatuni vya dhihaka la
Charlie Hebdo na mtu mwingine ambaye alishiriki katika mauaji hayo aliwakamata
mateka watu kadhaa katika duka la Wayahudi akijaribu kuwasaidia ndugu hao
kutoroka.
Ghasia
mbaya kabisa za kigaidi nchini Ufaransa kuonekana kwa miongo kadhaa
zimesababisha kuuwawa kwa kiasi ya watu 20, ikiwa ni pamoja na watu hao watatu
waliokuwa na silaha. Mshukiwa na nne, mke wa mtu aliyeshambulia katika eneo la
soko, bado anatafutwa na anaaminika kuwa ana silaha.
Kesho Jumapili kutakuwa na
mkusanyiko mkubwa mjini Paris kuwakumbuka wahanga wa shambulio hilo ambapo
viongozi kadhaa watahudhuria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni