Kiasi cha Shilingi bilioni 2 kimetumika
kukamilisha ujenzi wa barabara katika vijiji vya Mamba Myamba na Mpinji vilivyopo katika Jimbo la Same Mashariki
mkoani Kilimanjaro huku wananchi wa kipongeza hatua hiyo.
Wakizungumza walisema tangu nchi ipate
Uhuru mwaka 1961 walikuwa wakiteseka kutokana na kukosekana kwa huduma
mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara.
“Tunamshukuru sana Rais Kikwete kwa
kutujengea barabara hizi, kwetu sisi wananchi imekuwa faraja kubwa, kukamilika
kwa barabara hizi kutafungua fursa nyingi ambazo zitakuwa chachu ya maendeleo
katika vijiji vyetu,” walisema wananchi hao.
Mmoja wa wakazi wa Mamba Myamba, Elieti
Kikoro alisema walikuwa wakilazimika kubeba mizigo yao kichwani au kwa kutumia
wanyama kama punda kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu hususani
kipindi cha masika.
Alisema kujengwa kwa barabara hizo kumekuwa
mkombozi mkubwa kwa wananchi waishio milimani katika jimbo hilo ambalo
hawakutegemea kama siku moja watakuwa na barabara ambayo itawezesha kusafirisha
mazao yao.
Diwani wa Kata ya Mamba Myamba, Michael
Chikira alisema kukamilika kwa barabara hiyo kutasaidia kufungua fursa za kiuchumi
na wananchi wataweza kuzalisha kwa wingi zao lao la tangawizi na kuinua pato la
taifa.
Alisema barabara hiyo ilianza kujengwa
kufuatia ombi lililotolewa kwa Rais Kikwete na Mbunge wa jimbo la Same
Mashariki Anne Kilango Malecela, ambao Rais Kikwete aliaahidi kutekeleza ombi
hilo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo,
Anne Kilango Malecela alisema kujengwa kwa barabara hizo ni msaada mkubwa kwa
wananchi waishio maeneo ya milimani katika jimbo hilo.
Aidha Kilango aliongeza kuwa barabara
hizo zenye urefu wa Kilometa 13.8, zimegharimu kiasi cha shilingi bilioni
mbili, na kwamba maeneo zilizopojengwa barabara hizo ni barabara ya Parame
Kitubwa-Korogwe Mpinji (Km 8.7), na Kiwandani Manga-Chalinze (Km 4.8).
Tunataka kujua ukubwa wa km za mraba za Tarafa ya Mamba Vunta
JibuFuta